Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, Japhet Lusingu |
MAHABUSU Watatu waliokuwa wanapelekwa katika Gereza la Butimba, jijini Mwanza, wakitokea kijiji cha Nyang`amango wilayani Misungwi, wamefariki dunia wakati wakijaribu kuwanyang`anya Polisi silaha.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Japhet Lusingu, amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo, ambapo amesema, Ebina Muhono, Mkazi wa Mkuyuni jijini hapa, alikufa papo hapo baada ya kuruka kutoka kwenye gari la Polisi namba PT. 1680 Land Cruiser.
Amesema wengine wawili, Daniel Elias na Maramba Range, wao walipata majeruha baada ya kuanguka wakati wakijaribu kuruka na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi na walifariki dunia jana asubuhi.
Lusingu amesema katika tukio hilo ambalo lilitokea Julai 23 Mwaka huu saa 10:30 jioni, mahabusu mmoja, Denis Mahuti, Mkazi wa Tarime alifanikiwa kutoroka akiwa chini ya ulinzi wa sajenti, Mahamoud.
“Mahabusu hao ghafla walijaribu kuwapora askari silaha waliokuwa wakiwasindikiza katika gereza la Butimba lakini Polisi walipambana na watuhumiwa na kushindwa kuwapora silaha,” amesema Lusingu.
Hata hivyo amesema watuhumiwa wote wanne wanatuhumiwa kwa kesi za unyang`anyi wa kutumia silaha ambazo ni CC. 27 na 30 za Mwaka 2015 katika Mahakama ya Wilaya ya Misungwi.
Wakati huo huo, watu wanne wanaodaiwa kuwa majambazi waliokuwa na silaha idhaniwayo ni SMG/ SAR wamevamia boti ya Mv. Zenegathe na kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Charles.
Kamanda Lusingu amesema tukio hilo lilitokea Julai 23 Mwaka huu, saa 9:00 katika kisiwa cha Goziba kilichopo Mkoa wa Kagera na kisiwa cha Ghana.
No comments :
Post a Comment