Tuesday, July 21, 2015

MILIPUKO YA MABOMU BUNJUMBURA KABLA YA UCHAGUZI

Kumetokea ufyatulianaji wa risasi na milipuko usiku kucha nchini Burundi, usiku wa kuamkia uchaguzi wa rais uliozua utata. Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo anawania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na katiba ya nchi.
Viongozi wengi wa upande wa upinzani wameapa kususia uchaguzi huo.
Saa chache tu kabla ya kufunguliwa shughuli ya upigaji kura, milipuko ya gruneti iliripotiwa jijini Bujumbura na kufuatiwa na milio ya risasi. Maeneo mengine risasi hizo zilisikika kwa wingi zaidi mjini humo. Japo haikuwa wazi ni nani hasa anayefyatua risasi hizo.
Kwa mujibu wa mshauri wa kisasa wa rais, haya ni mashambulio yanayofanywa na 'magaidi' wanaonuia kuvuruga shughuli ya uchaguzi.

Kumbu kumbu

Mnamo mwezi Mei, kundi la wanajeshi wa ngazi ya juu nchini Burundi walijaribu kufanya mapinduzi yaliyotibuka. Hata hivyo sasa baadhi yao wametishia kufanya shambulio lingine.
Hofu ya kuwa uchaguzi huu huenda ukalitumbukiza taifa hilo katika mzozo mbaya zaidi wa kisiasa imeifanya jamii ya kimataifa kuitisha kuahirishwa kwa uchaguzi na kupendekeza mashauriano ya amani.
Wito kama huu uliambulia patupu, mwishoni mwa wiki mashauriano ya amani yalivunjika na uchaguzi ndio huu unafanyika huku wito wa kuahirishwa kwake ukipuuziliwa mbali.
              null
Takriban watu 70 wamefariki katika maandamano ya awali kupinga uchaguzi huuhuku wengine zaidi ya elfu 160 wakiikimbia nchi kwa hofu ya kuzuka mapigano

No comments :

Post a Comment