Dar/Mikoani. Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Lucy Owenya amewabwaga makada wanane wa chama hicho, akiwamo Mkurugenzi wa Fedha wa Chadema, Anthony Komu katika kura za maoni kuwania ubunge Jimbo la Moshi Vijijini.
Wagombea wengine walikuwa ni Godlisten Malisa 6, Ekarist Kikiwia 5, Nicholaus Ngowi 3, Deogratius Munishi 1 na Joseph Nubi na Erneus Kyambo hawakupata kura.
Komu aliwaambia waandishi wa habari kuwa hakubaliani na matokeo hayo na atakata rufaa kulingana na kanuni na Katiba ya Chadema.
“Kwa kiwango kile cha kura nilichopata ni wazi kulikuwa na wizi au kupanga matokeo, Siyatambui matokeo haya,” alisema Komu.
Owenya aliwapongeza wapigakura kwa kutumia haki yao kuchagua kiongozi wanayemtaka bila kujali tofauti za kijinsia.
“Siasa za ubaguzi zimeshindwa. Wapigakura walikuwa wanawake na wanaume, wote wamenipa kura za kishindo,” alisema Owenya.
Hata hivyo, Malisa alisema uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki na wanachama walichagua mtu anayekubalika na kuuzika ndani na nje ya chama
Machemli achemsha
Aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe anayegombea ubunge kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mkundi amewashinda wagombea wenzake 10 baada ya kupata kura 232, kati ya kura 466 zilizopigwa.
Ushindi huo wa Mkundi ulimtia kiwewe Mbunge Salvatory Machemli aliyepata kura 74 kati ya 466.
Wagombea wengine waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Vitalius Charles aliyepata kura 4, Martin Malima 5, Daniel Mafuru na Clement Kanumi kura 6, Simon Mtobesya na Daud Tungaraza kura 9 kila mmoja.
Wagombea wengine ni Dk Majani Rwambari kura 59, Jacton Kulwijila 24 na Cletus Mnaku 71.
Kwa upande wa kura za maoni kwa wagombea wa ubunge viti maalumu zilizofanyika juzi, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (Mwanza), Sezalia Buyanza aliibuka kidedea kwa kupata kura 42.
Buyanza anayewania nafasi hiyo kwa tiketi ya Chadema, aliwashinda Sophia Donard aliyepata kura 36 na Joanita Lukiko 21. Majina yao yatapelekwa ngazi za juu za chama kwa hatua nyingine.
Kevela, Lwenge watupiana maneno
Mahasimu watatu wa kisiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Wanging’ombe, Gerson Lwenge na Yono Kevela wanachuana vikali kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama hicho kati ya wagombea 12.
Akiomba ridhaa ya kuchaguliwa na wanachama wa CCM ili apeperushe bendera ya chama hicho, Kevela alisema mwaka 2010 alishinda kwa kishindo, lakini chama kilimwengua na kumteua Lwenge kupeperusha bendera ya chama hicho.
Kwa upande wake Lwenge, alitumia muda huo kumtuhumu mpinzani wake akisema siyo mtu makini.
Blandes ajitoa kuombea
Wagombea wawili wa nafasi za ubunge katika Jimbo la Karagwe, wametangaza kujitoa kwenye kinyanganyiro hicho.
Walitangaza kutogombea nafasi hiyo katika mkutano wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Karagwe.
Wagombea hao ni Gosbert Blandes, ambaye ni Mbunge wa Karagwe kwa kipindi cha miaka 10 na Karim Amir, mjumbe wa mkutano mkuu Taifa wa CCM.
Wajumbe hao walisema wamefikia hatua hiyo kutokana na makundi makubwa waliyonayo, hivyo kuhofia kama wataendelea kugombea na anayetakiwa kupitishwa na kura za maoni ni mgombea mmoja, basi huenda wangeleta mpasuko katika chama.
Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Karagwe, Robert Runyoro alithibitisha kujiondoa kwa wagombea hao katika Jimbo la Karagwe.
Runyoro alisema baada ya tamko la wagombea hao chama hicho kilitoa taarifa katika uongozi wa chama ngazi ya mkoa.
Matokeo zaidi
Singida Magharibi: Marco Allute 171, Vicente Mghwai 16, Christowaja Mtinda 09, Hemedi Kulungu 7, Mdimi Mussa 1, Nkhangaa Ally 1 na Ngimba Aman 0.
Msalala: Paulo Ndundi 113, Peter Machanga 49, Ezekiel Kazimoto 48, Emmanuel Mbise 43, Francis Makune 15, Vincent Mhagwa 10, Richard Mabilika 1 na Stephen Bundala hakupata kura.
Butiama: Yusuf Kazi 202, Adam Taya 39, Issa Yusuf 31, Daniel Obeiya 3, Annicent Marwa 2, Lucas Ossoo 1 na Marto Yohana 1.
Nkasi Kaskazini: Keissy Sudi 158, Triphone Simba 70 na Stanley Khamsini 5.
Nkasi Kusini: Alfred Sotoka 70, Kaminga Hyporito 39, Emmanuel Sungura 9, Edson Ndasi 4 na Joseph Kitakwa 2.
Sumbawanga: Shadrack Malila 277, Kassian Kaegele 28, Musa Ndile 9, Matokeo Lyimo 1 na Eliud Mwasenga na James Kusula hawakupata kura.
Nachingwea: Dk Mahadhi Mmoto 207, Thomas Mmuni 99, Nurdin Mchora 28 na Ramadhani Chimbamga aliyepata kura 6.
Serengeti: Marwa Ryoba 280, Ramson Rutiginga 160, Maguye Simon 8, Mokoro Rugatiri 4 na John Mrema kura 1.
Dodoma Mjini: Benson Kigaila 155, Josephson Kihoja 20, Filbert Mhoja 1 na Emmanuel Npio hakupta kura.
Iramba Mashariki: Oscar Kapalale 87, Elia Gunda 55, Juma Mwanga 43 na George Gunda 33.
Kisesa: Masanja Manani 219, Masunga Ndemela 47, Sendama Hunge 16, Matondo Sebastian 4, Nkwabi Mahona 3, Erasto Tumbo na Simon Jilala walioambulia kura mbili kila mmoja.
Tabora. Peter Mkufya alishinda kwa kura 148, akifuatiwa na Profesa Nhomba Imajamasala 61, Said Mwasekela 51 na Maganga Raymond aliyepata kura 37.
Chemba: Kunti Majala alipita baada ya kupata kura 140, akifuatiwa na Longa Bura 40 na Issa Mtinange 14.
Busanda: Alphonce Mawazo 205, Finias Magesa 126 na Julius Marco 26.
Iramba Magharibi: Jesca Kishoa 121, Hassan Longoi 11 na Mary Almas 3.
Nkenge: Valelian Rugarabamu 156, Salimu Abubakary 82, Meshaki Nicus 18, Samuel Rumanyisa 17 na Thomas Matabaro 5.
Singida Mashariki: Tundu Lisu alipata kura zote za ndiyo 320.
Same Mashariki: Nagenjwa Kaboyoka 177, Onesmo Fue Fue 38, Nziacharo Makenya 3, Mchungaji Charles Kanyika 3 na Allan Mmasi 1.
Ilala: Naomi Kaihula 34, Muslim Hassanali 20, Joyce Mgela 14, Anderson Ndambo 2 na John Wangoma 1
Mkuranga: Baraka Mwago 88, Oyeiko Ngeleja 46, Olivia Mallonga 11 na Sifa Majura 10.
Bukoba Mjini: Wilfred Lwakatare 87, Kipara Masoud 53, Meza 18, Pereus 2, Matias Rweyemamu 2, Aidan Mganyizi 7 na Basheka Josephat 5
Lushoto: Mohamedi Mtoi 109 na Germano Mbelwa 13.
No comments :
Post a Comment