Sunday, July 26, 2015

NYAMBARI NYANGWINE ANG'AKA

Mbunge wa Jimbo la Tarime anayemaliza muda wake, Nyambari Nyangwine, amedai kuchezewa rafu akisema kuna baadhi ya vijana wamekuwa wakinywa
pombe aina ya viroba kwa ajili ya kumzomea ili aonekane hakubaliki kutetea nafasi yake.

Nyangwine ambaye anatetea nafasi yake kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa akigombea Tarime Vijijini, ametaka mchatako wa kumpata mgombea ambaye atapeperusha bendera ya CCM kuwania ubunge katika jimbo kufanyika kwa ustaarabu.
Alisema amelikemea jambo hilo katika vikao vya ndani huku akiwaomba wagombea wenzake kuheshiminiana na kuongeza kuwa angependa uchaguzi uwe huru na haki na kuwataka wagombea wenzake wasilazimishe kukubalika.
Hata hivyo, Nyangwine alisema ahadi alizitoa kwa wananchi wa Tarime katika uchaguzi wa mwaka 2010 zimetekelezwa kwa asilimia zaidi ya 90 na kwamba ana imani atashinda tena kwani wananchi wa Tarime wanaona kazi kubwa ambayo ameifanya katika kipidi chake cha miaka mitano.
Nyangwine alisema endapo atateuliwa tena kuwania ubunge atahakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo katika Jimbo la Tarime Vijijini.

No comments :

Post a Comment