BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), limetishia kufungua kesi dhidi ya wamiliki wa magari watakaogoma na
kusababisha usumbufu kwa wasafiri.
kusababisha usumbufu kwa wasafiri.
Tishio hilo limekuja baada ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) kusema kuwa kitaitisha mgomo endapo serikali haitapunguza ushuru wa mabasi kutoka asilimia 25 kufikia asilimia 10.
Akizungumza Dar es Salaam hivi karibuni, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Oscar Kikoyo alisema, wamepata taarifa ya mpango wa Taboa kuitisha mgomo huo, nakwamba, kisheria chama hicho hakina haki ya kufanya hivyo.
"Tumesikia kupitia vyombo vya habari kuwa utaitishwa mgomo. Tunaomba ieleweke kuwa Taboa si chama cha wafanyakazi kwa hicho, hakina haki ya kuitisha mgomo wa wafanyakazi. Ni Chama cha Wamiliki wa Mabasi".
Aliongeza kuwa, endapo mgomo utaitishwa, utakuwa batili na wao watakuwa na sababu ya msingi ya kumshitaki mmiliki mmoja mmoja alipe fidia wasafiri kwa hasara watakayokuwa wameipata.
Katika hatua nyingine, alisema Sumatra inatakiwa kukunjua kucha zake pia, kwa kuwachukulia hatua wamiliki hao wa mabasi, kutokana na uchochezi wa migomo ya mara kwa mara. Ushuru unaolalamikiwa na wamiliki wa mabasi ulianza kutozwa Julai Mosi, mwaka huu.
No comments :
Post a Comment