Friday, July 17, 2015

OBAMA HATOZURU KIJIJINI CHA BABA YAKE

#ObamainKenya ndilo neno linalotawala mitandao ya kijamii nchini Kenya huku rais huyo akitarajiwa kulitembelea taifa hilo.
Hatahivyo wakaazi wa kijiji cha Kogelo ambapo babaake Obama alizaliwa na kulelewa sasa
hawatalazimika kufanya maandalizi ya aina yoyote kufuatia ziara hiyo baada ya balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec kusema kuwa rais huyo hatozuru kijiji cha Kogelo.
''Ana mda mchache sana kwa hivyo basi atakuwa nairobi pekee'',alisema bwana Godec akizungumza na runinga ya KTN.
Bibiye Obama Sarah Obama alikuwa amejiunga na wakaazi wa Kogelo akimtaka Obama kuwatembelea kulingana na ripoti za kituo cha habari cha Capital fm,
Source: BBC Swahili

No comments :

Post a Comment