Friday, July 10, 2015

Ugiriki yatoa mapendekezo kujinusuru

Hatimaye Serikali ya Ugiriki imewasilisha mapendekezo yake ya kutafuta ukombozi wa mkopo kutoka kwa wadeni wake wa kimataifa.
Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kupandishwa kodi, mabadikilo katika mfumo wa malipo ya uzeeni na kupunguzwa matumizi ya serikali, yote,
yakiwa mambo yaliyopingiwa kura ya hapana katika kura ya maoni iliyofanywa siku ya Jumapili.
Ugiriki ilipewa hadi saa 6 usiku kuamkia ijumaa iwe imewasilisha mapendekezo hayo.
Mkuu wa Mawaziri wa fedha wa kundi la ukanda wa sarafu ya Euro, Jeroen Dijsselbloem , alisema mipango sasa itapitiwa kwa kina. Mapendekezo ni pamoja na kuongezeka kodi , mageuzi ya pensheni, kupunguzwa kwa matumizi na ahadi za ubinafsishaji. Arnold Kayanda na Maelezo Zaidi .
Source: BBC Swahili

No comments :

Post a Comment