Sunday, July 5, 2015

UREMBO: VYAKULA AMBAVYO VINAWEZA KUHARIBU RANGI NYEUPE YA MENO YAKO

 


 
Na Mchambuzi wa Mambo ya Urembo

  
Kama wewe ni mtu unayezingatia sana masuala ya urembo, umakini  ni suala la msingi sana hasa katka kuchagua aina ya vyakula. Uchaguzi huo haubakii kwenye kuangalia vyakula visivyonenepesha bali ata vyakula ambavyo vinaweza vikakuaribia muonekano wa meno yako.
 




"Nafikiri umeshawahi kukumbana na mtu mmoja au wawili au zaidi ambao hukuweza kuyaangalia meno yao mara mbili. "







Leo hii nimeamua kukupa "bonus topic " ya mambo yanayohusiana na meno. Kama tunavyojua meno ni sehemu muhimu sana ya urembo na muonekano, na ni kati ya kitu kinachokuonekana cha kwanza kabisa pale uapokutana na mtu kwa mara ya kwanza.
Wataalamu wa urembo wa meno kutoka jiji la New York nchini Marekani wamekuja na list ya vyakula ambavyo matumizi yake yanaweza yakasababisha kupotea kwa rangi na mng'ao wa meno yako na jinsi gani utaweza kudumisha mng'ao wa meno yako.
 
 

1. Kahawa

Kama wewe ni mpenzi wa kahawa hii inakuhusu. Wataalamu wanakushauri kutotumia kahawa plain badala yake uchanganye na maziwa ili kupoteza rangi ya kahawa. Hii nikwa sababu ukinywa kahawa " plain" rangi nyeusi ya kahawa inatabia ya kuchafua meno. Siyo hilo tu la kuchafua meno vile vile kahawa huwa na tabia ya kukausha mate hivyo ni kiasi kidogo sana cha mate kitabaki kwaajili ya kuondoa madoa yatakayo baki kwenye meno. Haya anayaongea Dr. Nancy Rosen, daktariwa meno kutoka Jiji la New York.

 

2. Vyakula vilivyosindikwa vyenye wanga

Vyakula vyenye wanga kama vile crakers, cookies, white bread (mikate ya ngano iliyokobolewa) na yakula vingine vilivyosindikwa havitachafua meno yako pekeyake bali husababisha ata meno kutoboka. Hii ni kwa sababu mara nyingi "snaks" zinakuaga na kiwango kikubwa cha sukari, na iwapo sukari hii itabaki kwenye meno kwa muda mrefu bakteria waliopo kwenye kinywa huitumia sukari hii na kutengeneza asidi ambayo husababisha meno kutoboka. Anasema Dr. Nancy Rosen

 

3. Red Wine (Wine nyekundu)

Rangi na asidi iliyopo kwenye wine nyekundu husababisha kulika kwa sehemu ya nje ya meno kitaalamu inaitwa "enamel erosion". Chenga chenga zilizopo kwenye wine nyekundu pia huchangia kwa kiasi kikubwa kuchafuka kwa meno, kwani hupenyeza na kuingia kwenye nafasi za meno. Anaelezea daktari wa meno Dr.Gregg Lituchy kutoka Lowenberg na Lituchy.
 
 
image

4.  Sosi ya nyanya (Tomato Sauce)

Sosi ya nyanya ni kati ya vyakula ambavyo vina kiwango kikubwa cha asidi ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha meno kuchafuka na kulika. Badala ya kutumia tomato sosi unashauriwa kutumia salads au kachumbari ili kuyalinda meno yakokuzuia yasichafuke
 
 
 
 

5. Chai

Majani ya chai yana asidi inayoitwa "tannic acid". Asidi hii inayotokana na mimea husababisha kwa kiwango kikubwa kuchafuka kwa meno hasa hasa katika sehemu ya nje. Unashauriwa kutumia green tea zaidi mbayo inahali ya alkali kuliko "black tea" ambayo inakiwango kikubwa cha asidi.
 
 
 
 
 

6. Achali 

Achali au kwa lugha ya kigeni (pickle) ni kati ya vyakula vyenye asidi nyingi. Kama tulivyoona vyakula vingine asidi ndiyo adui mkubwa wa meno kwani husababisha meno kulika na kuchafuka. Hivyo kama wewe ni mpenzi sana wa achali unashauriwa kupunguza matumizi yake na kuhakikisha unasafisha meno yako mara baaada ya kula achali. Kitu chamuhimu cha kuzingatia ni kwamba "usitumie dawa ya meno na mswaki, mara baada ya kula vyakula vyenye asidi au lugha ya kiswahili tindikali nyingi kwani kwa kitendo hichi unaweza ukasababisha kulika kwa sehemu ya nje ya meno, unashauriwa kusukutua kwa maji safi peke yake inatosha au subiri kwa saa moja kama unataka kutumia mswaki"
 
 

7. Zabibu na Berries

Zabibu nazo husababisha kuchafuka kwa meno kwa kiasi kikubwa. Zabibu na berries nazo huwa na kiwango kikubwa cha tindikali ambayo husababisha kuchafuka na kulika kwa meno
 
 
 
 
 
 

 

Hitimisho

 
Wataalamu wa meno na kinywa wanashauri matumizi ya mirija "straw" katika unywaji wa vinywaji vyenye asidi/ tindikali na rangi . Hii itasaidia katika kuyaweka meno mbali na vimiminika.
 
 

 

"JUMA PILI NJEMA"

 

No comments :

Post a Comment