Friday, July 17, 2015

Vazi la Burqa lapigwa marufuku Cameroon

Maafisa wa serikali kaskazini mwa Cameroon wamepiga marufuku wanawake kuvalia vitambara vinavyofunika nyuso zao maarufu kama Burka.

Uamuzi huo umechukuliwa kufuatia mashambulio ya mabomu yaliyotekelezwa na wanawake waliokuwa wamevalia Burka, wanaoaminika kuwa wafuasi wa kuni la Boko Haram.
Gavana wa jimbo la Far, amesema kuwa raia katika eneo hilo hawataruhusiwa kuendesha magari yenye vioo vilivyotundikwa karatasi maalum inayozuia watu kuona ndani.
Aidha uendeshaji wa piki piki umepigwa marufuku nyakati za usiku.
Siku ya Jumatano Gabon ilipiga marufuku wanawake kuvalia Burka hadharani na kazini kwa sababu ya mashambulio hayo yaliyofanyika nchini Cameroon.
Mwezi uliopita Chad pia ilipiga marufuku wanawake kuvalia Burka.
Source: BBC Swahili

No comments :

Post a Comment