" Madhara kama haya hayajaonesha kuwapata wanaume, na imeendelea kuwa hivyo hata baada ya watafiti kuondoa sababu ya kutokufanya mazoezi"
Kukaa kwa muda mrefu
kunaweza kunaongeza hatari ya wanawake kupata kansa ya maziwa pamoja na kansa ya damu, suala ambalo limekua ni tofauti kwa wanaume ambao kukaa kwa muda mrefu hakuwa sababishii kupata tatizo hili, utafiti mpya unaonyesha.
Kama ilivyoripotiwa kwenye jarida liitwalo journal Cancer Epidemiology, Biomarkers & Prevention, utafiti ulifanyika kwa kuwafuatilia watu zaidi ya 146,000 wanawake na wanaume ambao hawakuwa na kansa wakati utafiti unaanza. Ufuatiliaji ulianza mwaka 1992 mpaka 2009.
Katika kipindi hicho takribani washiriki 31,000 walipata kansa.
Kukaa kwa muda mrefu kunasababisha ongezeko la hatari ya kupata kansa kwa asilimia 10 kwa wanawake, kitu ambacho hakijaonekana kwa wanaume. Aina ya kansa zilizoonekana kujionyesha ni kansa ya damu na kansa ya maziwa.
Utafiti vile vile unaonyesha kwamba ufanyaji wa mazoezi unaweza kupunguza hatari ya kupata kansa.
No comments :
Post a Comment