Tuesday, July 14, 2015

VIDEO: MAJAMBAZI YAVAMIA KITUO CHA POLISI SITAKI SHARI

Dar es salaam: Askari wa nne wa Jeshi la Polisi na raia watatu wamefariki dunia  katika tukio la ujambazi lililotokea katika kituo cha Polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga jijini Dar es Salaam.
 
Katika tukio hilo watu wapatao nane wamesadikika kuingia katika kituo hicho cha Polisi eneo la Stakishari majira ya saa 4 usiku wa kuamkia jana.
 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu amesema lengo la la watu hao ni kutaka kuiba silaha zilizokuwa katika kituo hicho cha Stakishari.
 
Aidha, amesema wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zinazohusu uharifu kwa Jeshi la Polisi.
 
Pia, kuhusu uvamizi wa Majambazi, Mangu amesema watajitahidi kuanza kuimarisha ulinzi kwa upande wao hususani katika vituo vya Polisi ndiyo baadae kwenda kuimarisha usalama wa  wananchi.

No comments :

Post a Comment