Dodoma. Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye pia alikuwa mwanamkakati katika kambi ya Edward Lowassa katika mbio za urais, amesema kambi
yake inamuunga mkono mgombea urais aliyeteuliwa na chama kwa sababu anauzika.
Dk Nchimbi alisema Dk John Magufuli ni mgombea anayeuzika tofauti na wengine na kwamba kambi yao inamuunga mkono katika kukiwezesha chama kuendelea kushika dola.
Alisema linapofika suala la maslahi ya chama wote wanakuwa kitu kimoja na kwamba uwezo na utendaji wa Dk Magufuli ni wa hali ya juu, kiasi kwamba ni rahisi kumnadi kwa wananchi.
Dk Nchimbi ambaye baada ya Kamati Kuu kutangaza majina matano ya wanaowania kuteuliwa, yeye na wajumbe wenzake wawili wa Kamati Kuu, Sophia Simba na Adam Kimbisa walitoka hadharani wakisema wanajitenga na maamuzi ya kamati hiyo kwa kuwa imekiuka katiba ya CCM.
Alisema baada ya vikao vya CCM kumpitisha Dk Magufuli, kambi yao imeamua kumuunga mkono kwakuwa ni mtendaji mzuri wa kazi anazopewa na mifano ipo mingi katika wizara alizoziongoza.
Dk Nchimbi alitoa mifano ya utendaji wa Dk Magufuli kwa kuwa ameweza kujenga barabara, kukamata meli za kigeni zinazovua kwa njia haramu katika bahari ya Tanzania na kupambana na ujenzi usiofuata sheria hasa kwenye maeneo ya barabara.

No comments :
Post a Comment