Thursday, July 2, 2015

Watu wanne wafariki Dunia Baada ya Basi Kugonga Treni

 
Watu wanne wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa  sku ya Jumanne baada ya basi aina ya Isuzu kugonga treni ya abiria  iliyokuwa ikienda bara kati ya stesheni ya Kimamba na Kilosa Mkoani Morogoro. Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11:25 asubuhi,
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elia Mshana imesema basi hilo lenye namba za usajili T 837 CTM Isuzu Coaster linamilikiwa na Feisal A. Khuwel wa Kilosa.
 
Taarifa kutoka eneo la tukio imefafanua kuwa waliofariki ni wanaume wawili, mwanamke mmoja na mtoto wa miaka minne. Kwa upande wa majeruhi, majeruhi 21 wako wanaume 14 na wanawake 7 ambao wanaendelea na matibabu katika Hospital ya Wilaya ya Kilosa.
 
Hata hivyo baada ya ajali treni ya abiria imeondoka katika stesheni ya Kilosa saa 3 asubuhi kuendelea na safari yake kwenda Bara

No comments :

Post a Comment