Wednesday, July 1, 2015

UTENGENEZAJI WA JAMU YA NANASI


 




Na. Emanuel Cosmas

UTANGULIZI

Jamu ya nanasi ni bidhaa inayotengenezwa kwa kutumia mchanganyiko wa mananasi yaliyosagwa (pulp) na kuchemshwa pamoja na sukari na acid. Ili kupata jamu yenye ubora mzuri ni sharti kuzingatia uwiano mzuri kati ya acid, sukari na pectin.

 

Mahitaji/Viambaupishi:


Nanasi
Sukari

 




 

 

    

 

citric acid (Kutegemeana na aina ya matunda)


   Vifaa:


·        Sufuria

·        Kijiko cha chai

 

·        Visu

·        Kipima joto (thermometer)

 

·        Chujio

·        Mwiko

 

·        Ndoo

·        Sinia

·        Refractometer

 

·        Mzani

·        Mashine ya kusaga matunda (blender)au ‘pulper’

 

·        Ubao wa kukatia matunda


Hatua za uzalishaji

  1. Osha matunda vizuri kwa maji safi na salama. Chagua matunda yalyoiva
  2. Menya matunda na ondoa macho na moyo wa katikati, katakata vipande na uvizage.
  3. Chemsha kupata pulp ya matunda
  4. Weka sukari
  5. Weka acid
  6. Changanya vizuri, pika polepole ukikoroga hadi joto la kutosha litakapofikia.
  7. Hakikisha jamu yako imeiva vizuri
  8. Jaza kwenye chupa safi ikiwa bado ya moto.
  9. Jamu tayari
 
END.

1 comment :

  1. Post nzuri, lakini hukusema sukari kiasi gani na citric acid kiasi gani. Nieleweshe hapo

    ReplyDelete