CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimempumzisha Katibu Mkuu wake
Dk. Wilbroad Slaa. Aidha, wanachama wake wametakiwa kuacha kuwa hofu kutokana na ujio wa Lowassa kwa kuogopa kunyanganywa vyeo vyao na wafuasi wake.
Mbowe amesema, “inawezekana Slaa naye anahofu juu ya ujio wa Lowassa kama ilivyo kwa wanachama wengine, wakidhani kuwa nafasi zao zitachukuliwa na wananchama wapya”. Hayo yanabainishwa leo Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Freeman Mbowe alipokuwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
“Katika hatua zote hizo tulikuwa sambamba na Slaa lakini baadae alibadilika ghafla na kutofautiana na Kamati kuu.Na mimi mwenyewe binafsi jana nimekaa nae zaidi ya masaa mawili nikijaribu kuongea nae lakini hatukufikia muafaka” amesema Mbowe.
Amesema maamuzi hayo ya kumpumzisha Slaa yameamuliwa na Kamati kuu ya Chadema baada ya kuwa katika mazungumzo ya muda mrefu bila kupata muafaka wa hatima ya ukimya wake.
Akizungumza na waandishi kabla ya kuanza Mkutano wa Baraza Kuu Chadema Mbowe amesisitiza kuwa Slaa alibadilika ghafla baada ya Kikao Cha Kamati Kuu.
Mbowe ameeleza kuwa, awali Chama kilikaa vikao vingi kujadili juu ya ujio wa Waziri mstaafu Edward Lowassa kujiunga na Chadema na kufikia makubaliano yaliyowahusisha viongozi wote wa Chama akiwemo Slaa.
Mbowe amesema, chama hakiwezi kusimama kufaya shughuli zake kikisubiri maamuzi ya mtu mmoja hivyo kitaendelea na kazi zake hususani katika kipindi hiki kigumu cha uchaguzi.
Mbali na hilo, amesema, “Chama kipo tayari kumpokea wakati wowote atakapokuwa tayari kurudi katika nafasi yake na sisi bado tunampenda na kumheshimu kama kiongozi”
“Leo nimeamua kuweka wazi suala hili baada ya kusikia na kuona vyombo vya habari mbalimbali vikiripoti habari zisizo za kweli ya kwamba Slaa amejiuzu na kwamba Chama kimempora mali zake na kumtishia habari hizo sizakweli na wala chama hakina ugomvi nae”.
Amesema, wanachama hawatakiwi kuhofia chochote juu ya ujio wa Lowassa na wafuasi wake kwani Chadema ni chama cha wananchi kwa yoyote atakae hitaji kujiunga anakaribishwa.
“Lakini hofu hii haipo kwetu tu ipo hata kwao Chama cha mapinduzi (CCM) kwani hawajawahi kupata hofu na viboko kama hivi vya kuondokewa na wafuasi wengi tena kwa wakati mmoja kama mwaka huu”.
Amesema CCM hadi sasa bado hawajielewi kutokana na mapigo mengi yaliyowapata kutokana na kuondokewa na kada wao mkubwa, na wengine bado wanakuja na hii ndio furaha ya chadema ili kuweza kuimaliza CCM Oktoba Mwaka huu.
“Ni lazma tuitumie fursa hii tuliyoipata na hatuwezi kuiacha. Lengo letu ni kuwa na wafuasi wengi zaidi haswa kutoka CCM ili tuzidi kuwamaliza kabisa tumeshawapokea wengi na tutazidi kuwapata wengi zaidi”.
Akizungumzia mkutano mkuu utakaofanyika kesho katika ukumbi wa Mlimani city Dar, ambapo amesema utamtangaza rasmi mgombea urais kwa tiketi ya Chadema pamoja na kumtangaza mgombea mwenza wa chama hicho.
No comments :
Post a Comment