Monday, August 3, 2015

HICHI NACHO NI MUHIMU KUFAHAMU


Je, wewe ni mpenzi wa chipsi kuku, nyama ya kuku n.k? Je ni kuku wa aina gani unawatumia? Unafahamu kwamba kuna baadhi ya wafanyabiashara na wakulima wa
chakula ambao hufanya uchakachuzi wa bidhaa kwa lengo la kuziba (mask) ubora halisia wa chakula husika kwa na kupunguza gharama za uzalishaji na mwisho wa siku kumuibia mteja kwa kuifanya bidhaa kuonekanana ubora usiokuwa na uhalisia.

Kuna mambo mengi sana ambayo hutendeka kwa siri hasa kwenye sekta ya vyakula ambayo iwapo ukiambiwa unaweza usiamini. Leo ntaongelea sekta ya nyama ya kuku kwani na mimi ni mpenzi wa kuku pia. Kwenye sekta ya nyama kuku kunavingi huwa vinafanyika ili leo nitaongelea viwili matumizi ya Steroid pamoja na Matumizi ya Maji na Chumvi iitwayo Polyphosphates.

Matumizi ya Polyphosphates


Chumvi chumvi aina ya polyphosphates hudungwa kwenye nyama ya kuku sehemu mbalimbali kuongeza uwezo wa nyama ya kuku kuhifadhi maji na hivyo mwiso wa siku kuongeza uzito wa nyama ya kuku...
Je, Ulikua unalifahamu hilo? 
Mara nyingi bei ya kuku hutegemeana na uzito au ukubwa wa kuku mwenyewe...Kuku mkubwa---uzito mkubwa---Bei kubwa.

Polyphosphates hutumika kwa lengo kuifanya nyama ya kuku isipoteze maji wakati wa uandaaji mpaka inapokufikia mlaji.
 Mara nyingi asilimia tano (5%) ndicho kiwango kinachotakiwa lakini baadhi ya wafanya biashara wasiokuwa waaminifu huweka iwango kikubwa zaidi pamoja na maji mengi ili kuiongeza uzito wa kuku kwa kiwango kikubwa. 



Mara nyingi kuku waliofanyiwa maujanja  au uhuni huu hupoteza uzito kwa kiasi kikubwa wakati wa mapishi au kupika. Video ifuatayo inaonyesha jinsi ambavyo wizi huo unafanyika;


Vitendo hivi vya kuchoma nyama ya kuku sindano zenye mchanganyiko wa chumvi chumvi za polyphosphate na maji vilianza kufanyika toka miaka ya 1970. 

Kihalisia hakuna mzalishaji au mkulima atakaye kuambia kwamba kuku wao wamewapiga hizo sindano, na ni vigumu pia kwa mlaji kutambua kwamba kuku wanao wanunua wamepigwa sindano kwani mara nyingi vitu hivi havionyeshwi moja kwa moja kwenye label  husika. Si hivyo tu bali ata kuku wenyewe mara nyingi tunawanunua wakiwa hawana vifungashio. 
Kwa kupitia label tu na sheria kali ndiyo itakua msaada kwa mlaji.
Matumizi ya Steroids

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani (U. S FDA) matumizi ya homoni za steroid kama vile estrogen, progesterone, testosteron yalianza tangu miaka ya 1950. mamlaka za Vyakula na Dawa(FDA) ziliruhusu matumizi ya homoni za steroid kwa wanyama kama vile ng'ombe na kondoo. 
Homoni hizi hutumika kwa lengo la kuongeza kasi ya ukuaji na kufanya wanyama waongezeke uzito kwa kasi kwa kukibadilisha chakula wanachokula kuwa nyama.
 Homoni hizi pia huongeza uzalishaji wa maziwa kwa wanyama. Mamlaka ziliruhusu matumizi hayo kwa kuwa kuliaminika kwamba chakula wanachokula kuku ni salama kwa binadamu na madawa hayo hayamdhuru mnyama husika na mazingira yao.

 Homoni za steroid hutumika kwa lengo la kuwafanya wanyama waongezeke uzito kwa haraka hivyo kutoa nyama ya kutosha au nyingi kwa haraka. Mara nyingi homoni hizi hubaki kwenye nyama za mifugo hivyo kunauwezekano mkubwa wa kumletea madhara mtumiaji wa nyama husika. Baadhi ya madhara anayoweza kuyapata binadamu ni pamoja na;





Watoto kuvunja ungo kabla ya wakati (Early Puberty in Girls)

Kwa mujibu wa Chuo Kikuu cha Cornell, ni kwamba matokeo ya tafiti nyingi bado zimetoa majibu ambayo bado yanakinzana hivyo ni vigumu kuelezea moja kwa moja madhara ambayo mtu anaweza kuyapata akiwala hao kuku waliokuzwa kwa steroid. 

Ingawa baadhi ya watafiti wanasema kwamba matumizi ya 'Steroid hormon' huweza kuwasababishia watoto wa kike kuvunja ungo mapema zaidi. na vilevile inaweza ikawa ni kisababishi kikubwa cha kansa ya matiti ukubwani. Kutokana na hili ushauri unatolewa wa watu kuachana na matumizi ya vyakula vyenye steroid.

Kansa ya matiti


Watafiti wanasema kwamba kisababishi kikubwa cha kansa ya matiti ni homoni kwenye yakula. 


Kwa mujibu wa mtaalamu wa afya Andrew Weil, M.D.mabaki ya hormoni kwenye vyakula husabaisha kuongezeka kwa uweekano wa kupata kansa ya maziwa. Kwa baadhi ya nchi kama vile Marekani matumizi ya homoni katika kukuzia wanyama kama vile Kuku na Bata mzinga yamekatazwa.Ingawa matumizi ya hormon hizi yanatumiwa kwa wanyama wengine kma vile ng'ombe na kondoo.

 Kama unataka kuondokana na hormon hizi ni vyema kuchunguza label kwa umakini na kuhakikisha kwamba zimandikwa, "no hormones administered." hususani kwa bidhaa zilizotoka nje ya nchi. Kibongo bongo ni vigumu kudhibiti kwani utaratibu wa kupaki vyakula haufanyiki kwa kiasi kikubwa.

Njia ya kugundua kuku aliyeongezewa maji na chumvi chumvi (Polyphosphate)

Kwa mujibu wa Dr. Patrick Otto (WHO) kuna njia rahisi zinazoweza kutumika ili kugundua uhalifu huu. Njia mojawao ni kumuweka kuku aliyegandishwa kwenye sehemu ya joto la kawaida (room temperature) na kuangalia kiasi cha maji kitakachotoka kwenye kuku husika kadiri barafu  zitakavyokua zinayeyuka na kulinganisha uzito wa kuku kabla na baada ya barafu kuyeyuka.

 Kwa kuku wa kawaida kiasi kidogo cha maji kinatakiwa kuzalishwa na hakutakiwi kuwa na utofauti mkubwa wa uzito, kabla na baada.

Hitimisho:

Kutokana na mambo haya kufanyika kwa vificho, wakati mwingine ni vigumu sana kwa mtu kufahamu kinachotendeka. Licha ya mazingira haya bado nafasi ipo hasa kwa mamlaka zinazohusika kuhakikisha zinawabana waingizaji wa bidhaa mbalimabli za vyakula nchini na kuwafuatilia wazalishaji wa ndani na nje kwa ukaribu kwani michezo kama hii inaweza fanywa na mzalishaji yeyote wa nje na  hata wa ndani.

 Kwa mujibu wa Dr. Kapela, ni muhimu sana kwa ukaguzi kufanywa husuani kwa wafugaji na wauzaji wa vyakula hasa kwenye hoteli za mitaani pamoja na vibanda vya chipsi ingawa kunauwezekano mkubwa wa michezo hii kufanywa zaidi kwa kuku wanaoingizwa kutoka nje zaidi ya wanaozalishwa ndani (Sina experience sana kama ukaguzi unafanyika kwenye mahoteli makubwa)


KAZI NI KWAKO!!!


No comments :

Post a Comment