Saturday, August 8, 2015

CHENGE AWA MWIBA KWA SEKRETARIETI YA MAADILI

Mbunge wa Baruadi Mgharibi, Andrew Chenge (kushoto) akipangua hoja za mwanasheria wa serikali aliyembele ya mwenyekiti wa Tume ya Maadili.
BARAZA la Sekretariati ya Maadili Tanzania imetoa siku tatu kuwasilisha faili la madai kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Andrew Chenge anaeshutumiwa kupokea sh1.6
bilioni kutoka kampuni ya VIP Engeneering and Marketing Limited. Baraza hilo lilijadili juu ya tuhuma hizo leo Jijini Dar es Salaam e s salaam lililoongozwa na Mwenyekiti Jaji Hamisi Msumi.


Chenge alitoa utetezi wake na kusema malipo aliyoyapata yalikuwa ni kwaajili ya ushauri na si kwa sababu yeye ni kiongozi wa umma na alikiri kupokea fedha hizo zikiwa ni malipo ya kutoa ushauri na si vinginevyo.

Chenge amesema aliingia mkataba na kampuni hiyo kwa kutoa ushauri wa kisheria dhidi ya kampuni ya mechmer ambazo ni kampuni binafsi, na kueleza kuwa hakuna kifungu cha sheria kinachomzuia kutoa ushauri kwa kampuni binafsi kisheria.

Kufikia uwamuzi wa mawakili watatu wa serikali kuwasilisha karatasi za madai kwa Chenge baada ya chenge kuomba kubadilishiwa tarehe iliyopangwa ya mawakili hao ya kumuwasilishia madai hayo tarehe 14 mwezi huu hadi jaji Msumi aliomba mawakili kuwasilisha tarehe 11.

Baada ya majaji hao Getrude Cykiacus, Filosticus Manula na Hassan Mayunga kuwasilisha madai hayo kwa kwenye Baraza hilo mnamo tarehe 11 mwezi huu, atafuatia Mbunge wa Bariadi mashariki (Andrew Chenge)kurudisha majibu ya madai hayo mnamo tarehe 14 mwezi huu.

No comments :

Post a Comment