Mgombea wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli (pichani), leo anatarajia kuchukua fomu ya kugombea kiti hicho katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(Nec), jijini Dar es Salaam.
(Nec), jijini Dar es Salaam.
Dk. Magufuli atasindikizwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula, Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es Salaam, baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu na makada wengine.
Ratiba hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipozungumza na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa Nnauye, Dk. Magufuli ataondoka ofisi ndogo za CCM saa tano asubuhi akiambatana na viongozi mbalimbali na wanachama kwa kupitia barabara ya Morogoro, Bibi Titi, Ohio hadi ofisi za Nec kwa ajili ya kuchukua fomu.
Nnauye alisema baada ya Dk. Magufuli kuchukua fomu atarejea ofisi za CCM kwa ajili ya kuzungumza na wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho mchana.
Wakati huo huo, Nnauye amesema vikao vya juu vya chama vinatarajia kuanza kesho kutwa Agost 6, mwaka huu kwa ajili ya kujadili na kupitisha majina ya wagombea nafasi za ubunge.
Alisema Agost 6 hadi 7 kutakuwa na kikao cha Kamati Maalum Zanzibar. Agost 8-9 kutakuwa na kikao cha Sekretarieti, Agost 10 hadi 11 kikao cha Kamati Kuu na Agost 12 hadi 13 kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho itakutana ambayo itakuwa na kazi ya jkufanya uteuzi rasmi.
Dk. Magufuli ataambana na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan, kwenda kuchukua fomu hizo.
No comments :
Post a Comment