Sunday, August 9, 2015

MAPISHI YA KEKI

Keki ni moja kati ya vyakula jamii ya mkate na ambavyo hutengenezwa kwa kuokwa. Kwa hivi sasa matumizi ya keki yamekua makubwa na muhimu sana kwani hutumika katika
matukio muhimu mbalimbali kama vile harusi, birthday na maadhimisho mbalimbali.



Viambata muhimu vinavyohitajika katika utengenezaji wa keki ni pamoja na unga wa ngano, sukari, mayai na mafuta. Viambata vingine vinavyoweza kuongezwa ni pamoja na maji pamoja na maziwa na vingine ambavyo husaidia katika kuumuka kwa keki ambapo baking powder au hamira.



Keki vile vile huweza kuongezew ladha mbali mbali kama vile ladha za matunda, vanilla etc.



Leo hii nakupa njia rahisi na haraka ya kutengeneza keki ambapo hautakua tena na haja ya kuenda kununua keki dukani au supermarket kwa ajili ya sherehe ndogo-ndogo.



Mahitaji

  • Unga wa ngano 1/4 kilo
  • Sukari 1/4 kilo
  • Blue band 1/4 kilo
  • Baking powder (kijiko kimoja cha chakula)
  • Mayai matano (5)
  • Ladha, Vanilla extract/ strawberry, lemon n.k kidogo kulingana na matakwa

Hatua za utengenezaji

  1. Changanya (sukari+blueband+mayai) weka pembeni (Tuite mchanganyiko wa kwanza)
  2. Changanya (unga+baking powder) weka pembeni(Tuite mchanganyiko wa pili)
  3. Changanya pamoja (mchanganyiko wa kwanza+mchanganyiko wa pili)
  4. Weka kwenye oven (seti nyuzi joto 150 C  ingawa itategemeana na jiko lilivyo) au unaweza ukaweka kwenye jiko la mkaa lenye moto kiasi juu na chini.
  5. Fuatilia uivaji wa keki mpaka inapokiwa ya brown
  6. Ili kujua kama keki imeiva unaweza ichoma katikati kwa kutumia kitu chenye ncha kali iwapo kitatoka kikiwa kikavu, keki imeiva...kama kitatoka na uji uji ujue bado

 

MWISHO

1 comment :