Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha kimesema viongozi ambao wameweka mguu mmoja CCM na mwingine upinzani na kuhujumu chama ni bora watoke mara moja wawaachie chama chao kuliko hujuma, vinginevyo watashughulikiwa.
Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha, Feruzy Bano, alisema wakati wa uchaguzi wa kura za maoni wamegundua hujuma zilizofanywa na baadhi ya viongozi wa CCM.
“Mfano unakuta wanachama wanatishwa na hasa maeneo ya Umasaini, na kusababisha wapiga kura kujitokeza wachache 7,251 kati ya wanachama hai 27,000,” alisema.
Alisema ni bora wakatoka wamfuate wanayemtaka kuliko kubaki wakati kimwili na roho hawako huko.
“Ila tupo katika uchunguzi baada ya muda si mrefu dawa yao inachemka maana wanajulikana,” alisema.
Aliwaonya wagombea nafasi ya udiwani waoshinda nafasi zao, ambao wana mpango wa kujitoa baadaye ili kuipa ushindi Chadema waache kufanya hivyo maana cha moto watakiona.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment