Mgombea wa Uraisi kupitia CCM Mh. John Pombe Magufuli amewatangazia kiama mafisadi, wezi na walarushwa.
Magufuli aliyaongea hayo Jana katika viwanja vya Jamhuri Manispaa ya Dodoma alipokua anakijitambulisha kwa wananchi waliokua wamefurika katika viwanja hivyo.
Akiwa mwenye kujiamini na mwenye bashasha na akishangiliwa na umati huo Wa wananchi Mh. Magufuli alisema kwamba atawashughulikia mafisadi wezi na walarushwa na hatowangusha wananchi.
Wengi wa wananchi waliosikiliza hotuba yake waliipongeza na kusema kwamba hotuba hiyo inatoa mwanga mpya hasa kutokana na kutokubagua wananchi kutokana na vyama vyao.
Mh. Magufuli alisisitiza kwamba hatowangusha wana CCM na Wapinzani (CHADEMA, CUF, NCCR n.k) na kuwaomba wamuamini na wampe ridhaa ya kuwaongoza.
No comments :
Post a Comment