Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe pamoja na Mbunge wa Nzega Dkt. Hamisi Kigwangalla wamekubali kushindwa katika kinyang’iro cha kuomba ridhaa ya kuteuliwa ndani ya chama cha Mapinduzi CCM zoezi lililohitimishwa leo.
Akizungumza na Mwandishi wetu mara baada ya Magufuli kutangazwa mshindi , Mh. Bernad Membe amesema angechaguliwa mtu mwingine pasinge tosha leo katika ukumbi mpya wa chama cha Mapinduzi CCM, lakini kuteuliwa kwa Dkt Magufuri ameridhika kabisa kutoka ndani ya moyo wake huku akimmwagia sifa Magufuli na kusisitiza kuwa watanzania wamepata mtendaji shupavu.
Naye Kigwangalla amesema hakika Magufuli ni chaguo la Mungu kwa kuwa ni mmoja kati ya wanasiasa ambao hawajatoa hata shilingi kumi kuwapa wadhamini ili adhaminiwe kama ilivyo kwa wanasiasa wengine.
Kwa mujibu wa Nape Nnauye katibu wa Itikadi na Uenezi CCM mara baada ya kumpata mwanasiasa atakaye peperusha bendera ya chama cha Mapinduzi amesema wanatarajia kufanya mkutano jijini Dar es salaam siku ya jumanne.
No comments :
Post a Comment